Je Wajua, UBUYU una Vitu Gani ambavyo ni Faida kubwa katika Mwili wako...? Twende Pamoja....

========================================
*******Tupate Elimu Chache Kuhusu Ubuyu*******
========================================
Ubuyu ni tunda ambalo hupatikana katika miti jamii ya adansonia. Ubuyu umekua na matumizi mbalimbali wengi tukiutumia kama matunda. Wengine hutumia juisi yake kutengenezea barafu (ice cream). Pia ili kuongeza ladha wengine huchanganya ubuyu na viungo mbalimbali ili kuongeza ladha ya ubuyu.
Figure 1: Wamama wakiwa wanaokota Mabuyu na kuweka katika Kapu
 
Vitu vyote vilivyomo kwenye mbuyu vinatumika kama chakula au dawa kwa faida ya binadamu.

FAIDA ZA UBUYU 

Kikubwa hasa ubuyu katika mwili una uwezo mkubwa wa kuimarisha kinga ya mwili, kuimarisha mifupa, kusaidia mfumo wa umeng’enyaji tumboni, kupunguza maumivu na uvimbe na kusisimua utengenezaji wa seli na tishu mpya . Pia kusaidia kupunguza shinikizo la damu na kuzuia magonjwa sugu.
Unga wa ubuyu unaelezwa kuwa na vitamini na madini mengi kuliko matunda mengine yoyote unayoyajuwa:-
1. Inaelezwa kuwa unga wa ubuyu una vitamini C nyingi mara 6 zaidi ya ile inayopatikana katika machungwa.
2. Ubuyu una kiwango kingi cha madini ya Kashiamu (Calcium) mara 2 zaidi ya maziwa ya ng’ombe, pia madini mengine yapatikanayo katika ubuyu ni pamoja na madini ya Chuma, Magnesiamu na Potasiamu ambayo ni mara 6 zaidi ya ile potasiamu ipatikanayo katika ndizi!
3. Husaidia kujenga neva za fahamu mwilini
4. Ina virutubisho vya kulinda mwili
5. Ubuyu una vitamini B3 na B2 ambayo ni mhimu katika kuondoa sumu mwilini na umeng’enyaji wa madini ya chuma, kimsingi vyakula vyenye afya zaidi kwa ajili ya mwili ya binadamu huwa pia huwa na vitamin B2.
6. Unaongeza kinga ya mwili sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamini C
7. Huongeza nuru ya macho
8. Husaidia kuzuia kuharisha na kutapika
9. Ina magnesiam ambayo husaidia kujenga mifupa na meno
10. Husaidia wenye presha ya kushuka na wenye matatizo ya figo

Figure 2: Ubuyu Baada ya kupasuliwa(Mbegu za Ubuyu)

Figure 3: Twanga Mbegu za Ubuyu ili kupata Unga wake
Matumizi na Viwango?
Jipatie kikombe kimoja cha juisi ya ubuyu kila siku hasa usiku na baada ya wiki kadhaa utaona matokeo yake mwilini.
Ili upate faida za juisi ya ubuyu, zinazoelezwa hapa, lazima upate ule ubuyu halisi (mweupe) usiochanganywa na kitu kingine cha kuongeza ladha au rangi.
Figure 4: Unga Wa Ubuyu

17 comments:

  1. Asante sana kwa elimu hii ya msingi yaani ya utambuzi wa vitu tunavyotumia kila siku, yaaani hii ni zaidi ya ELIMU kwani imenisaidia nielewe umuhimu wa Tunda hili kwa mapana yake, Ubarikiwe sana mkuu, Na Mola akujaalie uende zaidi ya hapa In Sha Allah.
    Ubarikiwe sana ndugu.

    ReplyDelete
  2. Nimejua mengi juu ya ubuyu na Sasa nitafanya kuwa chaguo language nilikuwa na uogopa mbuyu nikidhani ni hifadhi ya majini

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni safi sana kwani ni vyema kuimarisha kinga mwili zetu ili kujikinga na magonjwa mbalimbali.

      Delete
  3. Kwa Kweli tunakushukuru Sana kwa elimu nzuri ya afya na hasa juu ya matunda.
    Wengi hawajuwi umuhimu wa kutumia matunda tuliyo nayo Kila siku kwenye Miji yetu. Barikiwa na endelea kutuelimisha zaidi.

    ReplyDelete
  4. Asantee sana chief maana
    sana na sijui faida zake

    ReplyDelete
  5. Asante Sana kwa elimu nzuri yenye faida kubwa

    ReplyDelete
  6. Nimefurahi sana na natumia kwa faida yangu na MTOTO alie tumboni,MUNGU nisaidie

    ReplyDelete
  7. Sawa kabisa, hasara zake Ni zipi

    ReplyDelete
  8. Ni nzuri hata kutoa mning'inio wa ziada Kwa wapigaji gambe maana ukiiamka alfajiri ukapiga glass 1 ya juice isiyo na sukari baada ya muda unakua vzr kabisa., Sometimes unalamba hata Inga wake!!

    ReplyDelete
  9. Kwenye maelezo hujaainisha ni kiasi gani cha unga unatakiwa kuchanganya na maji,
    Na Je maji pendekezwa kutumia na unga ni maji ya moto au baridi?
    Ahsante

    ReplyDelete
  10. Juice ya ubuyu ni salama kwa mwenye presha ya kupanda??

    ReplyDelete
  11. Ahsante Sana kwa elimu hii,.nimejifunza sanaa

    ReplyDelete
  12. Asante kwa elimu hii Mungu akuzidishie🦅

    ReplyDelete
  13. Asante kwa elimu, vipi ukichanganya na sukari ni vizuri?

    ReplyDelete
  14. Habari jaman ubuyu usio na rangi unaharibika baada ya muda gan?

    ReplyDelete