Je, Papai ni nini?
Papai ni tunda la mpapai ("Carica papaya"), mti wa familia Caricaceae. Ni mti mrefu wenye shina la urefu wa mita 5 mpaka 10, wenye majani yaliojipanga yaliojizungusha na kujishikiza juu kwenye shina la miti, shina kwa upande wa chini huwa na makovu mengi kuonesha sehemu ambayo majani yalikuwa majani ya mpapai ni makubwa sm 50 – 70 kwa upana, maua yake ni madogo na hutokea sehemu yalipochomoza majani, hutengeneza tunda papai lenye urefu wa sm 15- 45, na upana wa sm10 – 30.
Tunda huiva pale linapokuwa laini ( kama vile parachichi au zaidi) na ngozi yake inapokuwa na ngozi yake inapo karibia rangi ya chungwa yaani njano, ladha ya chungwa hukamilana na ile kati ya nanasi na peasi, ingawa huwa ya utulivu bila ya uchungu wowote.
Figure 1: Juisi ya Papai (Sharubati ya Papai) |
Papai, tunda lenye ladha nzuri kama sukari, siyo tu ni tamu kulila, lakini ni chanzo kikuu cha virutubisho muhimu vinavyotoa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali, yakiwemo yale hatari ambayo huchukua maisha ya watu kila kukicha.
Leo soma faida za tunda hili ili ujiepushe na maradhi ambayo hutokea pale mwili unapokuwa na kinga ya mwili dhaifu kinga dhidi ya magonjwa ya moyo utaona kwamba maradhi ya moyo yana kinga karibu katika kila tunda au chakula cha asili.
Je Papai lina Faida gani katika miili yetu...?
Inaelezwa kuwa papai ni kinga ya ugonjwa wa moyo unaotokana na kuziba kwa mishipa ya damu (atherosclerosis ) na ule unaotokana na kupatwa na kisukari (diabetic heart disease). Kwa kula papai mara kwa mara, unajiepusha na magonjwa hayo yanayosababisha kifo haraka.
MFUMO USAGAJI CHAKULA
Papai pia limeonesha kuwa na uwezo mkubwa sana wa kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani ya utumbo ambayo hutokana na mtu kuwa na matatizo katika mfumo wake wa usagaji chakula. Papai huboresha mfumo mzima wa usagaji chakula na kumfanya mtu kupata choo laini na hivyo kujiepusha na madhara ya kukosa choo kwa muda mrefu ambayo humuweka mtu katika hatari ya kupatwa na kansa ya tumbo.
KINGA DHIDI YA UVIMBE NA VIDONDA
Watu wanaosumbuliwa na majipu au kutokewa na mauvimbe ya ajabu ajabu na kupatwa vidonda mara kwa mara, inatokana na kutokuwa na virutubisho muhimu ambavyo hupatikana kwenye tunda hili. Imegundulika kuwa, watu wenye matatizo hayo wanapotumia papai au virutubisho vyake, hupata nafuu haraka na kupona.
KINGA YA MWILI
Vitamin C na Vitamin A ambayo inapatikana mwilini kutokana na kirutubisho aina ya Ć¢beta-caroteneĆ¢ kilichomo kwenye papai, ni muhuimu sana kwa kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa yanayojirudia mara kwa mara kama vile mafua, maambukizi ya sikio, kikohoo, n.k
NURU YA MACHO
Kama karoti inavyoaminika katika kuimarisha nuru ya macho, papai nalo ni miongoni mwa tunda hilo. Imeelezwa kuwa watu wanaotumia tunda hili hujipa kinga madhubuti ya macho na pia kudhibiti kasi ya kuzeeka ambayo hutokana na kuongezeka kwa umri wa mtu.
TIBA YA MAPAFU
Kama wewe ni mvutaji sigara mzuri au mtu ambaye katika mazingira yako unayoishi unakumbana na moshi wa sigara, basi utumiaji wa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha vitamin A kama papai, kutakuepusha na kupatwa na madhara yatokanayo na moshi wa sigara.
SARATANI YA KIBOFU
Ulaji wa papai na chai ya kijani (green tea) kutakuepusha na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa saratani ya kibofu cha mkojo Utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa na Asia Pacific Journal of Clinical Nutrition umeeleza. Kwa faida hizi na nyingine, tupende kula tunda hili ili tujiepushe na magonjwa hatari yanayosumbua watu kila siku.
Maelezo ya ziada
-> Maziwa yanayotoka katika jani lake huponya vidonda. Pia yanasaidia kutibu kidonda cha moto.
Kama hiyo haitoshi, maziwa yanayotoka katika jani la mpapai yanatibu kiungulia na ugonjwa wa colon (njia ya haja kubwa ndani).
-> Pia husaidia kutofunga choo, maganda ya tunda la papai husaidia kutibu tatizo la kuungua, vipele na saratani ya ngozi.
-> Ukitafuna mbegu 10 – 12 kwa siku tano unaweza kutibu ini.
-> Ukimeza mbegu za papai kiasi cha kijiko cha chakula mara tatu kwa siku kama ulikuwa na homa inakwisha.
-> Ukizikausha ndani, kisha zikasagwa na kuwa unga, zinasaidia kutibu malaria.
-> Majani yake ukiyakaushia ndani, yanaweza kutibu pumu. Inapoanza kubana, yachome kisha jifukize, kule kubanwa kutaisha.
-> Pia yanasaidia kutibu shinikizo la damu.
Tumia kijiko kimoja cha chai, changanya na uji, kunywa mara tatu kwa siku tano.
Mizizi yake ikipondwa na kulowekwa katika maji yaliyochemshwa, lita mbili na nusu kwa dakika 15, yanatibu figo, na kuzuia kutapika. Kunywa nusu kikombe cha chai kutwa mara tatu kwa siku 5.
Figure 2: Papai Lenye Afya Njema Na Limeiva vyema |
0 comments:
Post a Comment