• Health/Afya

    Maelezo juu ya Afya yatakaa hapa

  • Fruits/Matunda

    Maelezo juu yaMatunda yatakaa hapa

  • Exercise/Mazoezi

    Maelezo juu ya Mazoezi yatakaa hapa

  • Mlo Kamili/ Balanced Diet

    Maelezo juu ya Mlo kamili

Je wajua Kuhusiana na Tunda Liitwalo PAPAI? Ni tunda la Aina gani na lina vitamin na virutubisho vya aina gani, na vinafaida gani katika miili yetu kwa ujumla wake..? Usiwe na shaka twende Pamoja kujifunza zaidi...

Je, Papai ni nini?

Papai ni tunda la mpapai ("Carica papaya"), mti wa familia Caricaceae. Ni mti mrefu wenye shina la urefu wa mita 5 mpaka 10, wenye majani yaliojipanga yaliojizungusha na kujishikiza juu kwenye shina la miti, shina kwa upande wa chini huwa na makovu mengi kuonesha sehemu ambayo majani yalikuwa majani ya mpapai ni makubwa sm 50 – 70 kwa upana, maua yake ni madogo na hutokea sehemu yalipochomoza majani, hutengeneza tunda papai lenye urefu wa sm 15- 45, na upana wa sm10 – 30.
Tunda huiva pale linapokuwa laini ( kama vile parachichi au zaidi) na ngozi yake inapokuwa na ngozi yake inapo karibia rangi ya chungwa yaani njano, ladha ya chungwa hukamilana na ile kati ya nanasi na peasi, ingawa huwa ya utulivu bila ya uchungu wowote.

Figure 1: Juisi ya Papai (Sharubati ya Papai)

Papai, tunda lenye ladha nzuri kama sukari, siyo tu ni tamu kulila, lakini ni chanzo kikuu cha virutubisho muhimu vinavyotoa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali, yakiwemo yale hatari ambayo huchukua maisha ya watu kila kukicha.

Leo soma faida za tunda hili ili ujiepushe na maradhi ambayo hutokea pale mwili unapokuwa na kinga ya mwili dhaifu kinga dhidi ya magonjwa ya moyo utaona kwamba maradhi ya moyo yana kinga karibu katika kila tunda au chakula cha asili.

Je Papai lina Faida gani katika miili yetu...?

Inaelezwa kuwa papai ni kinga ya ugonjwa wa moyo unaotokana na kuziba kwa mishipa ya damu (atherosclerosis ) na ule unaotokana na kupatwa na kisukari (diabetic heart disease). Kwa kula papai mara kwa mara, unajiepusha na magonjwa hayo yanayosababisha kifo haraka.

MFUMO USAGAJI CHAKULA
Papai pia limeonesha kuwa na uwezo mkubwa sana wa kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani ya utumbo ambayo hutokana na mtu kuwa na matatizo katika mfumo wake wa usagaji chakula. Papai huboresha mfumo mzima wa usagaji chakula na kumfanya mtu kupata choo laini na hivyo kujiepusha na madhara ya kukosa choo kwa muda mrefu ambayo humuweka mtu katika hatari ya kupatwa na kansa ya tumbo.

KINGA DHIDI YA UVIMBE NA VIDONDA
Watu wanaosumbuliwa na majipu au kutokewa na mauvimbe ya ajabu ajabu na kupatwa vidonda mara kwa mara, inatokana na kutokuwa na virutubisho muhimu ambavyo hupatikana kwenye tunda hili. Imegundulika kuwa, watu wenye matatizo hayo wanapotumia papai au virutubisho vyake, hupata nafuu haraka na kupona.

KINGA YA MWILI
Vitamin C na Vitamin A ambayo inapatikana mwilini kutokana na kirutubisho aina ya ‘beta-carotene’ kilichomo kwenye papai, ni muhuimu sana kwa kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa yanayojirudia mara kwa mara kama vile mafua, maambukizi ya sikio, kikohoo, n.k

NURU YA MACHO
Kama karoti inavyoaminika katika kuimarisha nuru ya macho, papai nalo ni miongoni mwa tunda hilo. Imeelezwa kuwa watu wanaotumia tunda hili hujipa kinga madhubuti ya macho na pia kudhibiti kasi ya kuzeeka ambayo hutokana na kuongezeka kwa umri wa mtu.

TIBA YA MAPAFU
Kama wewe ni mvutaji sigara mzuri au mtu ambaye katika mazingira yako unayoishi unakumbana na moshi wa sigara, basi utumiaji wa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha vitamin A kama papai, kutakuepusha na kupatwa na madhara yatokanayo na moshi wa sigara.

SARATANI YA KIBOFU
Ulaji wa papai na chai ya kijani (green tea) kutakuepusha na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa saratani ya kibofu cha mkojo Utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa na Asia Pacific Journal of Clinical Nutrition umeeleza. Kwa faida hizi na nyingine, tupende kula tunda hili ili tujiepushe na magonjwa hatari yanayosumbua watu kila siku.


Je Wajua, UBUYU una Vitu Gani ambavyo ni Faida kubwa katika Mwili wako...? Twende Pamoja....

========================================
*******Tupate Elimu Chache Kuhusu Ubuyu*******
========================================
Ubuyu ni tunda ambalo hupatikana katika miti jamii ya adansonia. Ubuyu umekua na matumizi mbalimbali wengi tukiutumia kama matunda. Wengine hutumia juisi yake kutengenezea barafu (ice cream). Pia ili kuongeza ladha wengine huchanganya ubuyu na viungo mbalimbali ili kuongeza ladha ya ubuyu.
Figure 1: Wamama wakiwa wanaokota Mabuyu na kuweka katika Kapu
 
Vitu vyote vilivyomo kwenye mbuyu vinatumika kama chakula au dawa kwa faida ya binadamu.

FAIDA ZA UBUYU 

Kikubwa hasa ubuyu katika mwili una uwezo mkubwa wa kuimarisha kinga ya mwili, kuimarisha mifupa, kusaidia mfumo wa umeng’enyaji tumboni, kupunguza maumivu na uvimbe na kusisimua utengenezaji wa seli na tishu mpya . Pia kusaidia kupunguza shinikizo la damu na kuzuia magonjwa sugu.
Unga wa ubuyu unaelezwa kuwa na vitamini na madini mengi kuliko matunda mengine yoyote unayoyajuwa:-
1. Inaelezwa kuwa unga wa ubuyu una vitamini C nyingi mara 6 zaidi ya ile inayopatikana katika machungwa.
2. Ubuyu una kiwango kingi cha madini ya Kashiamu (Calcium) mara 2 zaidi ya maziwa ya ng’ombe, pia madini mengine yapatikanayo katika ubuyu ni pamoja na madini ya Chuma, Magnesiamu na Potasiamu ambayo ni mara 6 zaidi ya ile potasiamu ipatikanayo katika ndizi!
3. Husaidia kujenga neva za fahamu mwilini
4. Ina virutubisho vya kulinda mwili
5. Ubuyu una vitamini B3 na B2 ambayo ni mhimu katika kuondoa sumu mwilini na umeng’enyaji wa madini ya chuma, kimsingi vyakula vyenye afya zaidi kwa ajili ya mwili ya binadamu huwa pia huwa na vitamin B2.
6. Unaongeza kinga ya mwili sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamini C
7. Huongeza nuru ya macho
8. Husaidia kuzuia kuharisha na kutapika
9. Ina magnesiam ambayo husaidia kujenga mifupa na meno
10. Husaidia wenye presha ya kushuka na wenye matatizo ya figo

Figure 2: Ubuyu Baada ya kupasuliwa(Mbegu za Ubuyu)

Figure 3: Twanga Mbegu za Ubuyu ili kupata Unga wake

Je Wafahamu Lolote Kuhusu Tunda Tango au Matango...?

================================================
Leo Tupate Kufahamu Faida Kumi za Tango katika Miili Yetu
================================================
Leo katika makala za kajamii tujifunze nakuzitambua faida za Tango katika miili yetu, ikiwa watu wengi tunakula bila kujua faida zake katika maisha ya kila siku. Watu wengi tunapenda matunda Fulani kwa ladha yake tuu bila kutaka kupata faida, Katika mwili ikiwa faida ya baadhi ya matunda ni pamoja na ladha yamatunda mbalimbali.

Jiunge nasi Katika kikundi cha Facebook

Figure 1: Matango(Tango)

FAIDA ZA TUNDA HILI KATIKA MIILI YETU
---------------------------------------------------------------------------------
1. Tango ni chanzo kizuri cha vitamin B.
2. Tango huupa mwili na vitamin. Asilimia 95 ya tango ni maji hivyo huupa mwili maji na kuusaidia kuondoa sumu mwilini kwani pia lina vitamin karibu zote ambazo mwili huhitaji kila siku.
3. Tango pia hutumika kwenye matunzo ya ngozi/urembo ambapo huwekwa machoni na kuondoa vimbe hasa kwa watu ambao umri umeanza kusogea kwani tango lina virutubisho vya kuondoa vimbe hizi na pia lina silicon na sulfur ambazo husaidia ukuwaji wa nywele.
4. Tango lina virutubisho kama lariciresinol, pinoresinol na secoisalariciresinol ambavyo kulingana na tafiti mbali mbali za magonjwa ya kansa husaidia kupunguza aina mbali mbali za kansa kama kansa ya matiti, kansa ya mifuko ya mayai kwa wanawake, kansa ya kizazi kwa wanawake na kansa ya tezi dume kwa wanaume.
5. Tango husaidia kuondoa harufu mbaya kinywani.
6. Tango huondoa hangover kwa watumiaji wa pombe kwani lina vitamin B ambazo husaidia kupunguza ukali wa maumivu ya kichwa pale unapoamka asubuhi ila unatakiwa kula kabla ya kulala ili uamke ukiwa vizuri.
7. Tango husaidia kupungua uzito na mmeng’enyo uende vizuri. Kutokana na kiasi kidogo cha sukari kilichopo kwenye tango na kiasi kikubwa cha maji, tango ni tunda sahihi kukusaidia upungue uzito. Kiasi cha maji kilichopo kwenye tango na Kamba Kamba zake huusaidia mwili kuondoa sumu katika mfumo wa chakula na kusaidia mmeng’enyo wa chakula. Unapokula tango kila siku pia hukusaidia wewe mwenye choo kigumu au usiyepata choo kabisa kwa muda mrefu kuondokana na tatizo hilo.
8. Tango husaidia wagonjwa wa kisukari, hupunguza mafuta mafuta kwenye mishipa ya damu na huweza kudhibiti shinikizo la damu aina zote mbili (Low and high blood pressure). Tango lina hormone ambayo huhitajika kwenye chembechembe za kongosho (pancreatic cells) ilikuweza kutengeneza insulin ambayo husaidia kudhibiti kiwango cha sukari kwenye mwili hivyo kuwasaidia wagonjwa wa kisukari. Pia watafiti wamegundua kuwa kuna kirutubisho kiitwacho sterol kwenye tango ambacho husaidia kupunguza mafuta kwenye mishipa ya damu. Tango lina kiwango kikubwa cha potassium, magnesium na Kamba Kamba ambazo husaidia sana kudhibiti shinikizo la damu aina zote yani high blood pressure na low blood pressure.
9. Husaidia afya ya viungo, huondoa gout na ugonjwa wa baridi yabisi (Arthritis). Tango ni chanzo kizuri cha silica ambayo inafahamika kusaidia afya ya viungo kwa kuimarisha viunganishi vya viungo (connective tissue). Pia tango lina Vitamin A, B1, B6, C & D, Folate, Calcium, Magnesium na potassium ambavyo hufanya tango linapochanganywa na juice ya karoti huweza kutibu gout na baridi ya yabisi (arthritis) kwa kupunguza kiwango cha tindikali kwenye mkoo (Uric acid).
10. Kutokana na maji na virutubisho vilivyopo kwenye tango, tunda hili husaidia kupunguza homa pale inapopanda.
Figure 2: Juisi ya Matango (Tango lililosagwa na kutengenezwa juisi yake)

Nadhani tutakuwa tumeelimika kwa kufahamu umhimu wa tunda aina ya tango ikiwa tunda hili halivutii kula kwa kuwa halina radha nzuri sana pia halina harufu inayosikia kuwa hili ni Tango kwa kukazia tango lina asilimia kubwa ya maji. 
Zingatia Madini ya Potassium yanayopatikana katika matango ndicho chakula cha moyo kwa sababu huwezesha moyo kupiga mapigo katika hali ya kawaida.
Figure 3: Tango Shambani/Katika Bustani

Ulaji wa matunda na vyakula vyenye kiwango kikubwa cha potassium kama tango ni muhimu sana hasa kwa mtu mwenye tatizo la moyo, shinikizo la chini la damu na pia kwa mtu asiye na tatizo la moyo hili kuimarisha ufanyaji kazi bora wa moyo.
😅😅😅