Wanawake wengi miaka ya karibuni wanakabiliwa na tatizo linalofanana na
kitambi kwa upande wa wanaume. Hivyo ingekuwa ni wanaume tungesema ni
kitambi ambalo nalo ni tatizo kubwa miongoni mwa wanaume wengi nyakati
za sasa.
Kinachowasumbuwa wanawake siyo kitambi tunasema ni
mrundikano wa mafuta sehemu ya chini ya tumbo na tumbo kwa ujumla
kufikia hali kuonekana kama ana tumbo kubwa au kuhisi labda ni ujauzito
kumbe ni mafuta tu mengi.
Kwa ujumla ni vigumu sana kupunguza
tumbo la namna hii, hivyo kwenye Makala hii pamoja na mengine tutaona pia
visababishi vya tatizo lenyewe, dawa za asili zinazoweza kuondoa tatizo
hilo na aina ya maisha unayotakiwa kuishi ili ufanikiwe kirahisi zaidi
bila kukuachia madhara mengine yoyote.
Nini kinasababisha tumbo kwa kina Mama(sio kwa kina Mama tu Bali ata kwa kina Baba:
Vyakula feki (Junk food)
Kutumia vyakula vya wanga kupita kiasi
Kutokunywa maji ya kutosha kila siku
Kula chakula kizito muda mchache kabla ya kwenda kulala(chakula chochote kinachohitaji mda mkubwa kumeng'enywa mfano Ugali, Chapati, Wali, nk)
Kukaa masaa mengi kwenye kiti
Kutokujishughulisha na mazoezi
Mfadhaiko (stress)
Kula wali kila siku
Ugali wa sembe
Kula vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi (chipsi, maandazi, nk)
NB:Tatizo linasababishwa na kula kitu kimoja kwa mda mrefu yaani karibu kila siku Bila kuchanganya na Milo ya Aina nyingine, vinavyoambatana na mazoea ya kila siku katika maisha kamakutojihusisha na mazoezi mbalimbali kama kutembea kwa umbali angalau kwa nusu saa kwa siku.
Ni tunda ambalo asili yake ni kutoka uarabuni asili ya uotaji wake ni katika Mazingira ya ukame yaani Jangwa. Tunda hili ni maarufu sana hususan kwa jamii ya kiislam, kutokana na utumikaji wa hali ya juu haswa katika kipindi cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, tende ndiyo tunda linaloliwa kwa
wingi, pengine kuliko tunda lingine. Tende hutokana na Mtende yaani tende ni tunda linalopatikana katika mti uitwao Mtende
"Tende ni Tunda na Mtende Ni Mmea aina ya kama Mnazi kwa muonekano"
Figure 1: Tende Kavu
Figure 2: Tende Mbichi
Je Ulaji wa Tende Una Faida Gani Katika Miili Yetu...?
Pamoja na kuwa ni tunda lenye ladha
tamu na nzuri mdomoni, lakini kisayansi pia limethibitika kusheheni madini na vitamini lukuki,
hivyo kuwa na faida nyingi kiafya
Na izi zifuatazo ni miongoni mwa Faida za Tende Katika Miili Yetu.
1. Ukila tende mara kwa mara, mwili wako utapata aina mbalimbali za
madini na vitamin za kutosha, ambazo zinapatikana kwenye tunda hili
maarufu duniani. Katika tende kuna kiasi kidogo tu cha mafuta (fat) na
haina lehemu (kolestrol).
2. Ukila tende, utajipatia kiasi cha
kutosha cha protini na vitamin B1, B2, B3, B5, A1, na C, virutubisho
ambavyo ni muhimu kwa ustawi wa afya ya mwili wako kwa ujumla.
3. Ulaji wa tende huimarisha na kuboresha mfumo wa usagaji chakula
tumboni, hivyo utaondokana na matatizo ya ukosefu wa choo, au matatizo
ya kupata choo kigumu kinachosababisha maumivu wakati wa kujisaidia. Pia
ndani ya tende kuna virutubisho vya ‘amino acids’ ambavyo ni muhimu
mwilini.
4. Ukila tende, mwili utapata nguvu na kukuondolea
uchovu ndani ya nusu saa tu, kwa sababu tende ina virutubisho vya sukari
asilia kama vile ‘glucose’, ‘sucrose’ na ‘fructose’. Ili kupata faida
zaidi za tende,
changanya na maziwa fresh kisha kula. Unapojisikia
mchovu, badala ya kunywa vinywaji baridi vinavyodai kuongeza nguvu, kula
tende, hata kiasi cha punje tatu kinatosha. Kwa wafunga saumu, ndiyo
maana inashauriwa kuanza kufungua kwa kula tende ili kuurejeshea mwili
wako nguvu iliyopotea siku nzima.
5. Tende ina madini pia aina
ya ‘potassium’ na kiasi kidogo cha chumvi (sodium). Madini haya husaidia
uimarishaji wa mishipa ya fahamu. Watafiti wamegundua kwamba ulaji
kiasi wa ‘potassium’ huweza kumuepusha mtu na kupatwa na kiharusi
(stroke). Pia tende husaidia kupunguza lehemu (cholesterol) mwilini (LDL
Cholesterol).
6. Kwa wale wenye matatizo ya ugonjwa wa kukauka
damu mwilini (anemia), wanaweza kupata ahueni kwa kula tende kwa wingi
ambayo ina kiwango cha kutosha cha madini ya chuma ambayo huhitajika
katika utengenezaji wa damu mwilini. Wakati vitu vitamu vingine huozesha
meno, utamu wa tende huzuia uozaji wa meno.
7. Kwa tatizo sugu na
la muda mrefu la ukosefu wa choo, loweka tende za kutosha kwenye maji
kiasi cha lita moja usiku kucha, kisha asubuhi changanya maji hayo
pamoja na hizo tende ili upate juisi nzito, kunywa na choo kitafunguka
na kuwa laini.
8. Kwa matatizo ya ukosefu wa nguvu za kiume,
mchanganyiko maalum wa tende, maziwa, asali na unga wa hiriki vinaweza
kuondoa tatizo lako. Chukua kiasi cha kiganja kimoja cha tende, loweka
kwenye maziwa ya mbuzi kiasi cha lita moja na yakae usiku kucha.
Asubuhi, zisage tende hizo kwenye maziwa hayo hadi zichangayike, kisha
weka asali kiasi cha vijiko vitatu au vinne vikubwa pamoja na unga wa
hiriki, kiasi cha nusu kijiko kidogo. Kisha kunywa mchangayiko huo kila
siku hadi utakapoona mabadiliko ya kuridhisha.
Figure 3: Juisi ya Tende
9. Tende ni dawa
ya unene, kwa wale wenye matatizo ya wembamba wa kupindukia na wanataka
kuongeza uzito, ulaji wa tende kila siku unaweza kuwasaidia. Lakini hii
ina maana kwamba, wale wanaohitaji kupunguza uzito, ulaji wa tende kwa
wingi hauwezi kuwafaa. Pia tende husaidia uondoaji wa kilevi mwilini.
10. Tende inatibu saratani ya tumbo. Habari njema kuhusu tende kama
tiba ni kwamba, haina madhara yoyote kwa sababu ni dawa asilia na
inafanyakazi vizuri kuliko dawa za ‘kizungu’. Tende vile vile ina
imarisha nuru ya macho na tatizo la kutokuona usiku (night blindness).
Tende ni tunda ambalo linayeyuka kirahisi tumboni na lenye faida nyingi
sana ambazo hulifanya liwe tunda la kipekee. Tunda hili limezoeleka
kuliwa wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ila sio mbaya ukapendelea
kula wakati wote kwani linafaida nyingi katika mwili.
Figure 4: Mtende wenye Tende(Mmea wa Tende na Matunda Yake)
Video ifuatayo inaelezea Faida za Tende na Dr. Zakir Naik
Chungwa ni tunda la mchungwa.
Ni kati ya matunda yanayovunwa sana duniani. Jina la kisayansi ni
Citrus aurantium L. var. sinensis L. au Citrus sinensis (L.) Osbeck.
Ni jamii ya matunda aina ya citrus. Jamii hii ya matunda inajumuisha machungwa, machenza, tangarine,
klementine n.k.
Tunda lenyewe ni kijani na rangi inabadilika kuelekea njano ikiiva. Pamoja na limau, danzi, balungi na ndimu ni mojawapo kati ya matunda chungwa. na yanapatikana kwa wingi na urahisi sehemu mbalimbali hapa nchini. Machungwa ni matunda maarufu sana sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania.
Asili yake ni katika Asia ya Kusini-Mashariki ambako lilioteshwa na wakulima.
Kuna aina mbili yanayotofautiana kwa ladha ama chungu au tamu.
Aina yenye ladha chungu iliwahi kusambaa duniani hivyo jina la
Kiswahili limetunza ladha hii hata kama matunda mengi yanayopandwa siku
hizi ni aina tamu.
Chungwa tamu lilisambaa kote duniani baada ya Wareno kuchukua machipuko yake na kuyapanda kwanza Ureno baadaye hata Amerika na Afrika kuanzia karne ya 15.
Figure 1: Chungwa Tunda na Juisi/Sharubati Yake
Virutubisho Vinavyoaptikana Katika Machungwa.
Machungwa yana mkusanyiko wa virutubisho vingi; Wanga, Protini kwa
kiasi kidogo, Vitamini (A, B1,B2,B3,B5,B6,B9, C, E) madini
(Kalsiam,Chuma, Zinki,Potasiam) na kambakamba (roughage/fibers).
Machungwa ni chanzo kikubwa na kizuri cha Vitamini C katika mlo.
Chungwa la ukubwa wa wastani lina miligramu 50 za Vitamini C, na kwa
kawaida mahitaji kwa siku ya Vitamini C ni miligramu 90 kwa mwanaume na
miligramu 75 kwa mwanamke. Hivyo chungwa moja au mawili kwa siku
yanaweza kutosheleza mahitaji hayo.
Machungwa yanaweza kuliwa kama tunda zima au kwa kunywa juisi ya
machungwa. Juisi ya machungwa huwa na virutubisho vyote vya machungwa
isipokuwa kambakamba (roughage/fibers), ambazo zipo kwa wingi zaidi mtu
napokula chungwa zima.
Figure 2: Machungwa yaliyovunwa tayari kwa matumizi mbalimbali
Kiwango cha asidi
Kama
ilivyo kwa jamii ya matunda ya citrus, machungwa nayo huwa na hali ya
aside, yenye kiwango cha pH karibu na 2.5 -3, kulingana na umri wake,
ukubwa na aina ya chungwa. Japo si kama ilivyo kwa limao, bado machungwa
huwa na kiwango cha asidi cha kutosha
Figure 3: Chati ya viwango vya PH
Je Ninapaswa Kula Machungwa Mangapi kwa siku?
Inashauriwa kula chungwa moja au mawili kwa siku, kwani hii
hutosheleza mahitaji ya Vitamin C na madini mengine mwilini. Ulaji wa
machungwa mengi sana(zaidi ya 50) kwa siku unaweza kusababisha kujaa
Vitamini C (hypervitaminosis) ambako ni hatari kwa afya. Kumbuka
kuwa hata chungwa moja tu ukila lina kidhi yale mahitaji muhimu ya
mwili ya kila siku (daily requirement), iwe chungwa lenyewe au juisi
yake halisi.
Figure 4: Chungwa Lililoiva Vyema
Faida za Machungwa:
Huimarisha Kinga ya Mwili.
Vitamini C pamoja na madini mengine ikiwemo Zinki, yanatumika kwenye ufanyaji kazi wa mfumo wa kinga ya mwili.
Hupunguza Hatari ya Magonjwa ya Moyo na Saratani.
Machungwa yana kampaundi ziitwazo phytochemicals kama hesperedin,
ambazo hulinda mishipa ya damu na kupunguza lehemu (cholesterol) kwenye
damu.Vitamini C pia iliyopo kwenye machungwa huondoa sumu za mwili (free
radicals), ambazo huchangia kutokea kwa saratani na magonjwa ya moyo
zinapokuwa zimelundikana mwilini.
Huimarisha afya ya fizi na mdomo.
Vitamini C husaidia kujenga protini za kolajeni za fizi za mdomoni,
hii huimarisha afya ya fizi. Ukosefu wa Vitamini C mara nyingi
huambatana na fizi kuvuja damu kutokana na kukosa protini za kolajeni za
kutosha.
Hupunguza lehemu(cholesterol) mwilini.
Machungwa yana kambakamba laini (soluble fibers) ambazo huyeyuka
kwenye chakula. Hizi husaidia kunyonya mafuta ya lehemu(cholesterol)
yaliyo kwenye chakula na kutolewa nje ya mwili kama choo. Hii hupunguza
mafuta ya lehemu(cholesterol) kwenye mwili wa mtu.
Kuona vizuri.
Machungwa yana Vitamini A ambayao inasaidia kuhakikisha macho yanaona
vizuri, pamoja na kamapundi nyingine ambazo hulinda tishu za macho
zisiharibiwe na mwanga.
Hupunguza hatari ya kukosa choo/kupata choo kigumu (constipation).
Machungwa hasa pale mtu anapokula chungwa zima, humpatia kambakamba
ambazo husaidia kulainisha chakula kwenye utumbo na kukifanya choo kuwa
laini.
Huimarisha afya ya ngozi.
Madini yaliyopo kwenye machungwa pamoja na Vitamini A na C husaidia kujenga na kuondoa seli za ngozi zilizokufa.
Fanya machungwa kuwa sehemu ya mlo wako kila siku ufaidike na kazi zake.
Papai ni tunda la mpapai ("Carica papaya"), mti wa familia Caricaceae. Ni mti mrefu wenye shina la urefu wa mita 5 mpaka 10, wenye majani
yaliojipanga yaliojizungusha na kujishikiza juu kwenye shina la miti,
shina kwa upande wa chini huwa na makovu mengi kuonesha sehemu ambayo
majani yalikuwa majani ya mpapai ni makubwa sm 50 – 70 kwa upana, maua
yake ni madogo na hutokea sehemu yalipochomoza majani, hutengeneza tunda
papai lenye urefu wa sm 15- 45, na upana wa sm10 – 30.
Tunda huiva pale
linapokuwa laini ( kama vile parachichi au zaidi) na ngozi yake
inapokuwa na ngozi yake inapo karibia rangi ya chungwa yaani njano, ladha ya chungwa
hukamilana na ile kati ya nanasi na peasi, ingawa huwa ya utulivu bila
ya uchungu wowote.
Figure 1: Juisi ya Papai (Sharubati ya Papai)
Papai, tunda lenye ladha nzuri kama sukari, siyo tu ni tamu kulila,
lakini ni chanzo kikuu cha virutubisho muhimu vinavyotoa kinga ya mwili
dhidi ya magonjwa mbalimbali, yakiwemo yale hatari ambayo huchukua
maisha ya watu kila kukicha.
Leo soma faida za tunda hili ili ujiepushe na maradhi ambayo hutokea
pale mwili unapokuwa na kinga ya mwili dhaifu kinga dhidi ya magonjwa ya
moyo utaona kwamba maradhi ya moyo yana kinga karibu katika kila tunda
au chakula cha asili.
Je Papai lina Faida gani katika miili yetu...?
Inaelezwa kuwa papai ni kinga ya ugonjwa wa moyo unaotokana na kuziba
kwa mishipa ya damu (atherosclerosis ) na ule unaotokana na kupatwa na
kisukari (diabetic heart disease). Kwa kula papai mara kwa mara,
unajiepusha na magonjwa hayo yanayosababisha kifo haraka. MFUMO USAGAJI CHAKULA
Papai pia limeonesha kuwa na uwezo mkubwa sana wa kutoa kinga dhidi ya
ugonjwa wa saratani ya utumbo ambayo hutokana na mtu kuwa na matatizo
katika mfumo wake wa usagaji chakula. Papai huboresha mfumo mzima wa
usagaji chakula na kumfanya mtu kupata choo laini na hivyo kujiepusha na
madhara ya kukosa choo kwa muda mrefu ambayo humuweka mtu katika hatari
ya kupatwa na kansa ya tumbo.
KINGA DHIDI YA UVIMBE NA VIDONDA
Watu wanaosumbuliwa na majipu au kutokewa na mauvimbe ya ajabu ajabu na
kupatwa vidonda mara kwa mara, inatokana na kutokuwa na virutubisho
muhimu ambavyo hupatikana kwenye tunda hili. Imegundulika kuwa, watu
wenye matatizo hayo wanapotumia papai au virutubisho vyake, hupata nafuu
haraka na kupona.
KINGA YA MWILI
Vitamin C na Vitamin A ambayo inapatikana mwilini kutokana na
kirutubisho aina ya Γ’beta-caroteneΓ’ kilichomo kwenye papai, ni
muhuimu sana kwa kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa
yanayojirudia mara kwa mara kama vile mafua, maambukizi ya sikio,
kikohoo, n.k
NURU YA MACHO
Kama karoti inavyoaminika katika kuimarisha nuru ya macho, papai nalo ni
miongoni mwa tunda hilo. Imeelezwa kuwa watu wanaotumia tunda hili
hujipa kinga madhubuti ya macho na pia kudhibiti kasi ya kuzeeka ambayo
hutokana na kuongezeka kwa umri wa mtu.
TIBA YA MAPAFU
Kama wewe ni mvutaji sigara mzuri au mtu ambaye katika mazingira yako
unayoishi unakumbana na moshi wa sigara, basi utumiaji wa vyakula vyenye
kiwango kikubwa cha vitamin A kama papai, kutakuepusha na kupatwa na
madhara yatokanayo na moshi wa sigara.
SARATANI YA KIBOFU
Ulaji wa papai na chai ya kijani (green tea) kutakuepusha na hatari ya
kupatwa na ugonjwa wa saratani ya kibofu cha mkojo Utafiti wa hivi
karibuni uliochapishwa na Asia Pacific Journal of Clinical Nutrition
umeeleza. Kwa faida hizi na nyingine, tupende kula tunda hili ili
tujiepushe na magonjwa hatari yanayosumbua watu kila siku.
========================================
*******Tupate Elimu Chache Kuhusu Ubuyu*******
========================================
Ubuyu ni tunda ambalo hupatikana katika miti jamii ya adansonia. Ubuyu
umekua na matumizi mbalimbali wengi tukiutumia kama matunda. Wengine
hutumia juisi yake kutengenezea barafu (ice cream). Pia ili kuongeza
ladha wengine huchanganya ubuyu na viungo mbalimbali ili kuongeza ladha
ya ubuyu.
Figure 1: Wamama wakiwa wanaokota Mabuyu na kuweka katika Kapu
Vitu vyote vilivyomo kwenye mbuyu vinatumika kama chakula au dawa kwa faida ya binadamu.
FAIDA ZA UBUYU
Kikubwa hasa ubuyu katika mwili una uwezo mkubwa wa kuimarisha kinga ya
mwili, kuimarisha mifupa, kusaidia mfumo wa umeng’enyaji tumboni,
kupunguza maumivu na uvimbe na kusisimua utengenezaji wa seli na tishu
mpya . Pia kusaidia kupunguza shinikizo la damu na kuzuia magonjwa sugu.
Unga wa ubuyu unaelezwa kuwa na vitamini na madini mengi kuliko matunda mengine yoyote unayoyajuwa:- 1. Inaelezwa kuwa unga wa ubuyu una vitamini C nyingi mara 6 zaidi ya ile inayopatikana katika machungwa. 2. Ubuyu una kiwango kingi cha madini ya Kashiamu (Calcium) mara 2 zaidi ya maziwa ya ng’ombe, pia madini mengine yapatikanayo katika ubuyu ni pamoja na madini ya Chuma, Magnesiamu na Potasiamu ambayo ni mara 6 zaidi ya ile potasiamu ipatikanayo katika ndizi! 3. Husaidia kujenga neva za fahamu mwilini 4. Ina virutubisho vya kulinda mwili 5. Ubuyu una vitamini B3 na B2 ambayo ni mhimu katika kuondoa sumu mwilini na umeng’enyaji wa madini ya chuma, kimsingi vyakula vyenye afya zaidi kwa ajili ya mwili ya binadamu huwa pia huwa na vitamin B2. 6. Unaongeza kinga ya mwili sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamini C 7. Huongeza nuru ya macho 8. Husaidia kuzuia kuharisha na kutapika 9. Ina magnesiam ambayo husaidia kujenga mifupa na meno 10. Husaidia wenye presha ya kushuka na wenye matatizo ya figo
Figure 2: Ubuyu Baada ya kupasuliwa(Mbegu za Ubuyu)
Figure 3: Twanga Mbegu za Ubuyu ili kupata Unga wake
================================================ Leo Tupate Kufahamu Faida Kumi za Tango katika Miili Yetu
================================================
Leo katika makala za kajamii tujifunze nakuzitambua faida za Tango katika miili yetu, ikiwa watu wengi tunakula bila kujua faida zake katika maisha ya kila siku.
Watu wengi tunapenda matunda Fulani kwa ladha yake tuu bila kutaka kupata faida, Katika mwili ikiwa faida ya baadhi ya matunda ni pamoja na ladha yamatunda mbalimbali.
FAIDA ZA TUNDA HILI KATIKA MIILI YETU
---------------------------------------------------------------------------------
1. Tango ni chanzo kizuri cha vitamin B.
2. Tango huupa mwili na vitamin. Asilimia 95 ya tango ni maji hivyo huupa mwili maji na kuusaidia kuondoa sumu mwilini kwani pia lina vitamin karibu zote ambazo mwili huhitaji kila siku.
3. Tango pia hutumika kwenye matunzo ya ngozi/urembo ambapo huwekwa machoni na kuondoa vimbe hasa kwa watu ambao umri umeanza kusogea kwani tango lina virutubisho vya kuondoa vimbe hizi na pia lina silicon na sulfur ambazo husaidia ukuwaji wa nywele.
4. Tango lina virutubisho kama lariciresinol, pinoresinol na secoisalariciresinol ambavyo kulingana na tafiti mbali mbali za magonjwa ya kansa husaidia kupunguza aina mbali mbali za kansa kama kansa ya matiti, kansa ya mifuko ya mayai kwa wanawake, kansa ya kizazi kwa wanawake na kansa ya tezi dume kwa wanaume.
5. Tango husaidia kuondoa harufu mbaya kinywani.
6. Tango huondoa hangover kwa watumiaji wa pombe kwani lina vitamin B ambazo husaidia kupunguza ukali wa maumivu ya kichwa pale unapoamka asubuhi ila unatakiwa kula kabla ya kulala ili uamke ukiwa vizuri.
7. Tango husaidia kupungua uzito na mmeng’enyo uende vizuri. Kutokana na kiasi kidogo cha sukari kilichopo kwenye tango na kiasi kikubwa cha maji, tango ni tunda sahihi kukusaidia upungue uzito. Kiasi cha maji kilichopo kwenye tango na Kamba Kamba zake huusaidia mwili kuondoa sumu katika mfumo wa chakula na kusaidia mmeng’enyo wa chakula. Unapokula tango kila siku pia hukusaidia wewe mwenye choo kigumu au usiyepata choo kabisa kwa muda mrefu kuondokana na tatizo hilo.
8. Tango husaidia wagonjwa wa kisukari, hupunguza mafuta mafuta kwenye mishipa ya damu na huweza kudhibiti shinikizo la damu aina zote mbili (Low and high blood pressure). Tango lina hormone ambayo huhitajika kwenye chembechembe za kongosho (pancreatic cells) ilikuweza kutengeneza insulin ambayo husaidia kudhibiti kiwango cha sukari kwenye mwili hivyo kuwasaidia wagonjwa wa kisukari. Pia watafiti wamegundua kuwa kuna kirutubisho kiitwacho sterol kwenye tango ambacho husaidia kupunguza mafuta kwenye mishipa ya damu. Tango lina kiwango kikubwa cha potassium, magnesium na Kamba Kamba ambazo husaidia sana kudhibiti shinikizo la damu aina zote yani high blood pressure na low blood pressure.
9. Husaidia afya ya viungo, huondoa gout na ugonjwa wa baridi yabisi (Arthritis). Tango ni chanzo kizuri cha silica ambayo inafahamika kusaidia afya ya viungo kwa kuimarisha viunganishi vya viungo (connective tissue). Pia tango lina Vitamin A, B1, B6, C & D, Folate, Calcium, Magnesium na potassium ambavyo hufanya tango linapochanganywa na juice ya karoti huweza kutibu gout na baridi ya yabisi (arthritis) kwa kupunguza kiwango cha tindikali kwenye mkoo (Uric acid).
10. Kutokana na maji na virutubisho vilivyopo kwenye tango, tunda hili husaidia kupunguza homa pale inapopanda.
Figure 2: Juisi ya Matango (Tango lililosagwa na kutengenezwa juisi yake)
Nadhani tutakuwa tumeelimika kwa kufahamu umhimu wa tunda aina ya tango ikiwa tunda hili halivutii kula kwa kuwa halina radha nzuri sana pia halina harufu inayosikia kuwa hili ni Tango kwa kukazia tango lina asilimia kubwa ya maji. Zingatia Madini ya Potassium yanayopatikana katika matango ndicho chakula cha moyo kwa sababu huwezesha moyo kupiga mapigo katika hali ya kawaida.
Figure 3: Tango Shambani/Katika Bustani
Ulaji wa matunda na vyakula vyenye kiwango kikubwa cha potassium kama tango ni muhimu sana hasa kwa mtu mwenye tatizo la moyo, shinikizo la chini la damu na pia kwa mtu asiye na tatizo la moyo hili kuimarisha ufanyaji kazi bora wa moyo.
π π π
The medical literature tells us that:- "The most effective ways to reduce the risk of heart disease, cancer, stroke, diabetes, Alzheimer's, and many more problems are through healthy diet and exercise" Our bodies have evolved to move, yet we now use the energy in oil instead of muscles to do our work.