• Health/Afya

    Maelezo juu ya Afya yatakaa hapa

  • Fruits/Matunda

    Maelezo juu yaMatunda yatakaa hapa

  • Exercise/Mazoezi

    Maelezo juu ya Mazoezi yatakaa hapa

  • Mlo Kamili/ Balanced Diet

    Maelezo juu ya Mlo kamili

 


Watu wengi hudhani kama mwanamke hapati ujauzito basi tatizo na lawama zote zitakuwa ni upande wa mwanamke, lakini hilo si lazima mara zote liwe hivyo. Kuna uwezekano mkubwa kuwa tatizo la kutopata mtoto katika familia likawa linatokana na ugumba upande wa mwanaume. Kwa tafiti zilizofanywa hivi karibuni zinaonesha kuwa wanaume wane(4) kati ya 10 wana tatizo la mbegu zao kuwa chache na kushindwa kutungisha mimba. Mwanaume kuzalisha mbegu chache kuliko kawaida ni mojawapo ya sababu kubwa za ugumba kwa wanaume.

Ili Mbegu ziwe chache zinatakiwa ziwe chini ya kiasi gani?

Shahawa kawaida ni mchanganyiko wa maji maji (ute) unaotengenezwa na tezi dume na mbegu za kiume (manii) zinazotengenezwa kwenye korodani. Mtu anakuwa na tatizo la mbegu chache pale katika kila millilita moja ya shahawa zake kunakuwa na mbegu (manii) chini ya millioni 20. Kwa kawaida mwanaume anazalisha zaidi ya manii millioni 20 katika kila millilita moja ya shahawa anazomwaga. Nadhani umenielewa vizuri sasa twende kwenye matibabu ya tatizo hilo

Mahitaji:

(i.)Majani mabichi ya mapera kilo moja  

(ii.)Kitunguu saumu robo kilo 

(iii.)Tangawizi robo kilo 

(iv.)Asali nusu lita.

Matayarisho na matumizi yake:

Katakata vitunguu saumu, tangawizi na majani ya mapera vipande vidogo vidogo sana kisha chemsha kwenye Maji Lita 3 na nusu kwa dakika 15 hadi 20, kisha acha ipoe na uchuje, chukua maji yako na uchanganye na asali yako kisha koroga vizuri kabisa. Mgonjwa anatakawa kunywa kikombe kimoja cha chai kutwa mara 2 kwa siku 7. 

Wakati wa kutumia dawa hii huruhusiwi kushiriki tendo la ndoa.πŸ‘‚πŸ‘‚πŸ‘‚πŸ™πŸ™πŸ™

Je Wajua Vyanzo halisi vinavyo pelekea Mtu kuwa na Tumbo Kubwa Mfano wa Mama Mjamzito..?

Je Ni kitambi ama ni Nini..?

Wanawake wengi miaka ya karibuni wanakabiliwa na tatizo linalofanana na kitambi kwa upande wa wanaume. Hivyo ingekuwa ni wanaume tungesema ni kitambi ambalo nalo ni tatizo kubwa miongoni mwa wanaume wengi nyakati za sasa.

Kinachowasumbuwa wanawake siyo kitambi tunasema ni mrundikano wa mafuta sehemu ya chini ya tumbo na tumbo kwa ujumla kufikia hali kuonekana kama ana tumbo kubwa au kuhisi labda ni ujauzito kumbe ni mafuta tu mengi.

Kwa ujumla ni vigumu sana kupunguza tumbo la namna hii, hivyo kwenye Makala hii pamoja na mengine tutaona pia visababishi vya tatizo lenyewe, dawa za asili zinazoweza kuondoa tatizo hilo na aina ya maisha unayotakiwa kuishi ili ufanikiwe kirahisi zaidi bila kukuachia madhara mengine yoyote.

Nini kinasababisha tumbo kwa kina Mama(sio kwa kina Mama tu Bali ata kwa kina Baba:

  • Vyakula feki (Junk food)
  • Kutumia vyakula vya wanga kupita kiasi
  • Kutokunywa maji ya kutosha kila siku
  • Kula chakula kizito muda mchache kabla ya kwenda kulala(chakula chochote kinachohitaji mda mkubwa kumeng'enywa mfano Ugali, Chapati, Wali, nk)
  • Kukaa masaa mengi kwenye kiti
  • Kutokujishughulisha na mazoezi
  • Mfadhaiko (stress)
  • Kula wali kila siku
  • Ugali wa sembe
  • Kula vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi (chipsi, maandazi, nk)
NB: Tatizo linasababishwa na kula kitu kimoja kwa mda mrefu yaani karibu kila siku Bila kuchanganya na Milo ya Aina nyingine, vinavyoambatana na mazoea ya kila siku katika maisha kamakutojihusisha na mazoezi mbalimbali kama kutembea kwa umbali angalau kwa nusu saa kwa siku.


Je wajua Tende(Dates) ina Faida Gani Mwilini Mwako...? Haswa unapotumia Mara Kwa Mara...?

TENDE NI NINI..?

 Ni tunda ambalo asili yake ni kutoka uarabuni asili ya uotaji wake ni katika Mazingira ya ukame yaani Jangwa. Tunda hili ni maarufu sana hususan kwa jamii ya kiislam, kutokana na utumikaji wa hali ya juu haswa katika kipindi cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, tende ndiyo tunda linaloliwa kwa wingi, pengine kuliko tunda lingine. Tende hutokana na Mtende yaani tende ni tunda linalopatikana katika mti uitwao Mtende

"Tende ni Tunda na Mtende Ni Mmea aina ya kama Mnazi kwa muonekano"

Figure 1: Tende Kavu

Figure 2: Tende Mbichi



Je Ulaji wa Tende Una Faida Gani Katika Miili Yetu...? 

Pamoja na kuwa ni tunda lenye ladha tamu na nzuri mdomoni, lakini kisayansi pia limethibitika kusheheni madini na vitamini lukuki, hivyo kuwa na faida nyingi kiafya

Na izi zifuatazo ni miongoni mwa Faida za Tende Katika Miili Yetu.
1. Ukila tende mara kwa mara, mwili wako utapata aina mbalimbali za madini na vitamin za kutosha, ambazo zinapatikana kwenye tunda hili maarufu duniani. Katika tende kuna kiasi kidogo tu cha mafuta (fat) na haina lehemu (kolestrol).

2. Ukila tende, utajipatia kiasi cha kutosha cha protini na vitamin B1, B2, B3, B5, A1, na C, virutubisho ambavyo ni muhimu kwa ustawi wa afya ya mwili wako kwa ujumla.

3. Ulaji wa tende huimarisha na kuboresha mfumo wa usagaji chakula tumboni, hivyo utaondokana na matatizo ya ukosefu wa choo, au matatizo ya kupata choo kigumu kinachosababisha maumivu wakati wa kujisaidia. Pia ndani ya tende kuna virutubisho vya ‘amino acids’ ambavyo ni muhimu mwilini.

4. Ukila tende, mwili utapata nguvu na kukuondolea uchovu ndani ya nusu saa tu, kwa sababu tende ina virutubisho vya sukari asilia kama vile ‘glucose’, ‘sucrose’ na ‘fructose’. Ili kupata faida zaidi za tende,
changanya na maziwa fresh kisha kula. Unapojisikia mchovu, badala ya kunywa vinywaji baridi vinavyodai kuongeza nguvu, kula tende, hata kiasi cha punje tatu kinatosha. Kwa wafunga saumu, ndiyo maana inashauriwa kuanza kufungua kwa kula tende ili kuurejeshea mwili wako nguvu iliyopotea siku nzima.

5. Tende ina madini pia aina ya ‘potassium’ na kiasi kidogo cha chumvi (sodium). Madini haya husaidia uimarishaji wa mishipa ya fahamu. Watafiti wamegundua kwamba ulaji kiasi wa ‘potassium’ huweza kumuepusha mtu na kupatwa na kiharusi (stroke). Pia tende husaidia kupunguza lehemu (cholesterol) mwilini (LDL Cholesterol).

6. Kwa wale wenye matatizo ya ugonjwa wa kukauka damu mwilini (anemia), wanaweza kupata ahueni kwa kula tende kwa wingi ambayo ina kiwango cha kutosha cha madini ya chuma ambayo huhitajika katika utengenezaji wa damu mwilini. Wakati vitu vitamu vingine huozesha meno, utamu wa tende huzuia uozaji wa meno.

7. Kwa tatizo sugu na la muda mrefu la ukosefu wa choo, loweka tende za kutosha kwenye maji kiasi cha lita moja usiku kucha, kisha asubuhi changanya maji hayo pamoja na hizo tende ili upate juisi nzito, kunywa na choo kitafunguka na kuwa laini.

8. Kwa matatizo ya ukosefu wa nguvu za kiume, mchanganyiko maalum wa tende, maziwa, asali na unga wa hiriki vinaweza kuondoa tatizo lako. Chukua kiasi cha kiganja kimoja cha tende, loweka kwenye maziwa ya mbuzi kiasi cha lita moja na yakae usiku kucha.

Asubuhi, zisage tende hizo kwenye maziwa hayo hadi zichangayike, kisha weka asali kiasi cha vijiko vitatu au vinne vikubwa pamoja na unga wa hiriki, kiasi cha nusu kijiko kidogo. Kisha kunywa mchangayiko huo kila siku hadi utakapoona mabadiliko ya kuridhisha.

Figure 3: Juisi ya Tende

9. Tende ni dawa ya unene, kwa wale wenye matatizo ya wembamba wa kupindukia na wanataka kuongeza uzito, ulaji wa tende kila siku unaweza kuwasaidia. Lakini hii ina maana kwamba, wale wanaohitaji kupunguza uzito, ulaji wa tende kwa wingi hauwezi kuwafaa. Pia tende husaidia uondoaji wa kilevi mwilini.

10. Tende inatibu saratani ya tumbo. Habari njema kuhusu tende kama tiba ni kwamba, haina madhara yoyote kwa sababu ni dawa asilia na inafanyakazi vizuri kuliko dawa za ‘kizungu’. Tende vile vile ina imarisha nuru ya macho na tatizo la kutokuona usiku (night blindness).

Tende ni tunda ambalo linayeyuka kirahisi tumboni na lenye faida nyingi sana ambazo hulifanya liwe tunda la kipekee. Tunda hili limezoeleka kuliwa wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ila sio mbaya ukapendelea kula wakati wote kwani linafaida nyingi katika mwili.

Figure 4: Mtende wenye Tende(Mmea wa Tende na Matunda Yake)


Video ifuatayo inaelezea Faida za Tende na Dr. Zakir Naik

Je Ninapaswa Kula Machungwa Mangapi kwa siku? Chungwa Lina Faida gani Mwilini?


Chungwa ni tunda la mchungwa. Ni kati ya matunda yanayovunwa sana duniani. Jina la kisayansi ni Citrus aurantium L. var. sinensis L. au Citrus sinensis (L.) Osbeck. Ni jamii ya matunda aina ya citrus. Jamii hii ya matunda inajumuisha machungwa, machenza, tangarine, klementine  n.k.
Tunda lenyewe ni kijani na rangi inabadilika kuelekea njano ikiiva. Pamoja na limau, danzi, balungi na ndimu ni mojawapo kati ya matunda chungwa. na yanapatikana kwa wingi na urahisi sehemu mbalimbali hapa nchini. Machungwa ni matunda maarufu sana sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania.

Asili yake ni katika Asia ya Kusini-Mashariki ambako lilioteshwa na wakulima. Kuna aina mbili yanayotofautiana kwa ladha ama chungu au tamu.
Aina yenye ladha chungu iliwahi kusambaa duniani hivyo jina la Kiswahili limetunza ladha hii hata kama matunda mengi yanayopandwa siku hizi ni aina tamu.
Chungwa tamu lilisambaa kote duniani baada ya Wareno kuchukua machipuko yake na kuyapanda kwanza Ureno baadaye hata Amerika na Afrika kuanzia karne ya 15.


Figure 1: Chungwa Tunda na Juisi/Sharubati Yake

Virutubisho Vinavyoaptikana Katika Machungwa.
Machungwa yana mkusanyiko wa virutubisho vingi; Wanga, Protini kwa kiasi kidogo, Vitamini (A, B1,B2,B3,B5,B6,B9, C, E) madini (Kalsiam,Chuma, Zinki,Potasiam) na kambakamba (roughage/fibers).
Machungwa ni chanzo kikubwa na kizuri cha Vitamini C katika mlo. Chungwa la ukubwa wa wastani lina miligramu 50 za Vitamini C, na kwa kawaida mahitaji kwa siku ya Vitamini C ni miligramu 90 kwa mwanaume na miligramu 75 kwa mwanamke. Hivyo chungwa moja au mawili kwa siku yanaweza kutosheleza mahitaji hayo.
Machungwa yanaweza kuliwa kama tunda zima au kwa kunywa juisi ya machungwa. Juisi ya machungwa huwa na virutubisho vyote vya machungwa isipokuwa kambakamba (roughage/fibers), ambazo zipo kwa wingi zaidi  mtu napokula chungwa zima.

Figure 2: Machungwa yaliyovunwa tayari kwa matumizi mbalimbali

Kiwango cha asidi
Kama ilivyo kwa jamii ya matunda ya citrus, machungwa nayo huwa na hali ya aside, yenye kiwango cha pH karibu na 2.5 -3, kulingana na umri wake, ukubwa na aina ya chungwa. Japo si kama ilivyo kwa limao, bado machungwa huwa na kiwango cha asidi cha kutosha
Figure 3: Chati ya viwango vya PH


Je Ninapaswa Kula Machungwa Mangapi kwa siku?
Inashauriwa kula chungwa moja au mawili kwa siku, kwani hii hutosheleza mahitaji ya Vitamin C na madini mengine mwilini. Ulaji wa machungwa mengi sana(zaidi ya 50) kwa siku unaweza kusababisha kujaa Vitamini C (hypervitaminosis) ambako ni hatari kwa afya.
Kumbuka kuwa hata chungwa moja tu ukila lina kidhi yale mahitaji muhimu ya mwili ya kila siku (daily requirement), iwe chungwa lenyewe au juisi yake halisi.

Figure 4: Chungwa Lililoiva Vyema


Faida za Machungwa:
  • Huimarisha Kinga ya Mwili.
Vitamini C pamoja na madini mengine ikiwemo Zinki, yanatumika kwenye ufanyaji kazi wa mfumo wa kinga ya mwili.
  • Hupunguza Hatari ya Magonjwa ya Moyo na Saratani.
Machungwa yana kampaundi ziitwazo phytochemicals kama hesperedin, ambazo hulinda mishipa ya damu na kupunguza lehemu (cholesterol) kwenye damu.Vitamini C pia iliyopo kwenye machungwa huondoa sumu za mwili (free radicals), ambazo huchangia kutokea kwa saratani na magonjwa ya moyo zinapokuwa zimelundikana mwilini.
  • Huimarisha afya ya fizi na mdomo.
Vitamini C husaidia kujenga protini za kolajeni za fizi za mdomoni, hii huimarisha afya ya fizi. Ukosefu wa Vitamini C mara nyingi huambatana na fizi kuvuja damu kutokana na kukosa protini za kolajeni za kutosha.
  • Hupunguza lehemu(cholesterol) mwilini.
Machungwa yana kambakamba laini (soluble fibers) ambazo huyeyuka kwenye chakula. Hizi husaidia kunyonya mafuta ya lehemu(cholesterol) yaliyo kwenye chakula na kutolewa nje ya mwili kama choo. Hii hupunguza mafuta ya lehemu(cholesterol) kwenye mwili wa mtu.
  • Kuona vizuri.
Machungwa yana Vitamini A ambayao inasaidia kuhakikisha macho yanaona vizuri, pamoja na kamapundi nyingine ambazo hulinda tishu za macho zisiharibiwe na mwanga.
  • Hupunguza hatari ya kukosa choo/kupata choo kigumu (constipation).
Machungwa hasa pale mtu anapokula chungwa zima, humpatia kambakamba ambazo husaidia kulainisha chakula kwenye utumbo na kukifanya choo kuwa laini.
  • Huimarisha afya ya ngozi.
Madini yaliyopo kwenye machungwa pamoja na Vitamini A na C husaidia kujenga na kuondoa seli za ngozi zilizokufa.

Fanya machungwa kuwa sehemu ya mlo wako kila siku ufaidike na kazi zake.
πŸ˜‡πŸ˜‡πŸ˜‡

Je wajua Kuhusiana na Tunda Liitwalo PAPAI? Ni tunda la Aina gani na lina vitamin na virutubisho vya aina gani, na vinafaida gani katika miili yetu kwa ujumla wake..? Usiwe na shaka twende Pamoja kujifunza zaidi...

Je, Papai ni nini?

Papai ni tunda la mpapai ("Carica papaya"), mti wa familia Caricaceae. Ni mti mrefu wenye shina la urefu wa mita 5 mpaka 10, wenye majani yaliojipanga yaliojizungusha na kujishikiza juu kwenye shina la miti, shina kwa upande wa chini huwa na makovu mengi kuonesha sehemu ambayo majani yalikuwa majani ya mpapai ni makubwa sm 50 – 70 kwa upana, maua yake ni madogo na hutokea sehemu yalipochomoza majani, hutengeneza tunda papai lenye urefu wa sm 15- 45, na upana wa sm10 – 30.
Tunda huiva pale linapokuwa laini ( kama vile parachichi au zaidi) na ngozi yake inapokuwa na ngozi yake inapo karibia rangi ya chungwa yaani njano, ladha ya chungwa hukamilana na ile kati ya nanasi na peasi, ingawa huwa ya utulivu bila ya uchungu wowote.

Figure 1: Juisi ya Papai (Sharubati ya Papai)

Papai, tunda lenye ladha nzuri kama sukari, siyo tu ni tamu kulila, lakini ni chanzo kikuu cha virutubisho muhimu vinavyotoa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali, yakiwemo yale hatari ambayo huchukua maisha ya watu kila kukicha.

Leo soma faida za tunda hili ili ujiepushe na maradhi ambayo hutokea pale mwili unapokuwa na kinga ya mwili dhaifu kinga dhidi ya magonjwa ya moyo utaona kwamba maradhi ya moyo yana kinga karibu katika kila tunda au chakula cha asili.

Je Papai lina Faida gani katika miili yetu...?

Inaelezwa kuwa papai ni kinga ya ugonjwa wa moyo unaotokana na kuziba kwa mishipa ya damu (atherosclerosis ) na ule unaotokana na kupatwa na kisukari (diabetic heart disease). Kwa kula papai mara kwa mara, unajiepusha na magonjwa hayo yanayosababisha kifo haraka.

MFUMO USAGAJI CHAKULA
Papai pia limeonesha kuwa na uwezo mkubwa sana wa kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani ya utumbo ambayo hutokana na mtu kuwa na matatizo katika mfumo wake wa usagaji chakula. Papai huboresha mfumo mzima wa usagaji chakula na kumfanya mtu kupata choo laini na hivyo kujiepusha na madhara ya kukosa choo kwa muda mrefu ambayo humuweka mtu katika hatari ya kupatwa na kansa ya tumbo.

KINGA DHIDI YA UVIMBE NA VIDONDA
Watu wanaosumbuliwa na majipu au kutokewa na mauvimbe ya ajabu ajabu na kupatwa vidonda mara kwa mara, inatokana na kutokuwa na virutubisho muhimu ambavyo hupatikana kwenye tunda hili. Imegundulika kuwa, watu wenye matatizo hayo wanapotumia papai au virutubisho vyake, hupata nafuu haraka na kupona.

KINGA YA MWILI
Vitamin C na Vitamin A ambayo inapatikana mwilini kutokana na kirutubisho aina ya Γ’€˜beta-caroteneΓ’€™ kilichomo kwenye papai, ni muhuimu sana kwa kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa yanayojirudia mara kwa mara kama vile mafua, maambukizi ya sikio, kikohoo, n.k

NURU YA MACHO
Kama karoti inavyoaminika katika kuimarisha nuru ya macho, papai nalo ni miongoni mwa tunda hilo. Imeelezwa kuwa watu wanaotumia tunda hili hujipa kinga madhubuti ya macho na pia kudhibiti kasi ya kuzeeka ambayo hutokana na kuongezeka kwa umri wa mtu.

TIBA YA MAPAFU
Kama wewe ni mvutaji sigara mzuri au mtu ambaye katika mazingira yako unayoishi unakumbana na moshi wa sigara, basi utumiaji wa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha vitamin A kama papai, kutakuepusha na kupatwa na madhara yatokanayo na moshi wa sigara.

SARATANI YA KIBOFU
Ulaji wa papai na chai ya kijani (green tea) kutakuepusha na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa saratani ya kibofu cha mkojo Utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa na Asia Pacific Journal of Clinical Nutrition umeeleza. Kwa faida hizi na nyingine, tupende kula tunda hili ili tujiepushe na magonjwa hatari yanayosumbua watu kila siku.