Je Ni kitambi ama ni Nini..?
Wanawake wengi miaka ya karibuni wanakabiliwa na tatizo linalofanana na kitambi kwa upande wa wanaume. Hivyo ingekuwa ni wanaume tungesema ni kitambi ambalo nalo ni tatizo kubwa miongoni mwa wanaume wengi nyakati za sasa.Kinachowasumbuwa wanawake siyo kitambi tunasema ni mrundikano wa mafuta sehemu ya chini ya tumbo na tumbo kwa ujumla kufikia hali kuonekana kama ana tumbo kubwa au kuhisi labda ni ujauzito kumbe ni mafuta tu mengi.
Kwa ujumla ni vigumu sana kupunguza tumbo la namna hii, hivyo kwenye Makala hii pamoja na mengine tutaona pia visababishi vya tatizo lenyewe, dawa za asili zinazoweza kuondoa tatizo hilo na aina ya maisha unayotakiwa kuishi ili ufanikiwe kirahisi zaidi bila kukuachia madhara mengine yoyote.
Nini kinasababisha tumbo kwa kina Mama(sio kwa kina Mama tu Bali ata kwa kina Baba:
- Vyakula feki (Junk food)
- Kutumia vyakula vya wanga kupita kiasi
- Kutokunywa maji ya kutosha kila siku
- Kula chakula kizito muda mchache kabla ya kwenda kulala(chakula chochote kinachohitaji mda mkubwa kumeng'enywa mfano Ugali, Chapati, Wali, nk)
- Kukaa masaa mengi kwenye kiti
- Kutokujishughulisha na mazoezi
- Mfadhaiko (stress)
- Kula wali kila siku
- Ugali wa sembe
- Kula vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi (chipsi, maandazi, nk)
NB: Tatizo linasababishwa na kula kitu kimoja kwa mda mrefu yaani karibu kila siku Bila kuchanganya na Milo ya Aina nyingine, vinavyoambatana na mazoea ya kila siku katika maisha kamakutojihusisha na mazoezi mbalimbali kama kutembea kwa umbali angalau kwa nusu saa kwa siku.